(ABNA24.com) Rais Vladimir Putin wa Russia amepinga kutuhumiwa Iran kuwa ilihusika katika shambulizi dhidi ya kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa Televisheni ya Rusiya Al-Yaum, Putin amesema kuituhumu Iran kuhusu shambulizi ambalo haijahusika nalo si uadilifu na kuongeza kuwa yamkini dhulma hiyo ikapelekea kubadilika sera au muelekeo.
Rais Putin amesema nchi mbili za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu hazitaki vita na Iran. Aidha ameongeza kuwa, Russia iko tayari kusaidia katika kutatua matatizo ya eneo kupitia kuimarisha uhusiano wa Wairani na Waarabu.
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 14 2019, Kikosi cha Ndege Zisizo na Rubani (drone) za Jeshi na Makundi ya Kujitolea ya Wananchi wa Yemen, katika kujibu jinai za Saudia dhidi ya Wayemen, kilitumia drone 10 zilizoundwa na Wayemen katika kushambulia vituo vikubwa vya kusafisha mafuta vya Abqaiq and Khurais mashariki mwa Saudia ambavyo vinamilikiwa na shirika la Aramco.
Kufuatia mashambulizi hayo, Saudia ilishindwa kuuza asilimia 50 ya mafuta ghafi yake katika masoko ya dunia.
Marekani na waitifaki wake wamekuwa wakitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kudai kuwa Tehran ilihusika katika oparesheni hiyo ya Wayemen dhidi ya vituo hivyo vya mafuta vya Saudia. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha vikali kuhusika na mashambulizi hayo na imetaja madai dhidi yake kuwa yasiyo na msingi.
/129
14 Oktoba 2019 - 07:00
Msimbo wa Habari: 982508
Rais Vladimir Putin wa Russia amepinga kutuhumiwa Iran kuwa ilihusika katika shambulizi dhidi ya kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia.